Valencia asaini mkataba mpya Man United

Mchezaji wa pembeni wa Manchester United, Antonio Valencia amesaini mkataba mpya wa miaka minne ambao utamuweka Old Trafford hadi msimu wa mwaka 2015.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Antonio Valencia

Valencia mwenye umri wa miaka 25 amefunga mabao 10 katika mechi 69 tangu alipojiunga na Manchester United akitokea Wigan Athletic mwaka 2009.

Ameeleza katika mtandao wa klabu hiyo: "Ninafuraha sana kubakia Manchester United. Natumai nitaendelea kukuza kipaji changu.

Mshambuliaji huyo wa pembeni raia wa Ecuador msimu uliopita alianza kucheza mechi nane tu baada ya kuvunjika kifundo cha mguu na hakuweza kuwemo katika kikosi cha timu yake kilichozuru Marekani hivi karibuni baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Lakini meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amefurahi kuweza kumbakisha Valencia kwa miaka minne ijayo.

"Antonio ametoa mchango mzuri sana tangu alipowasili katika klabu hii. Kasi yake, uwezo wa kuchonga krosi na wepesi wake vimekuwa ni vitu vya thamani kubwa kwetu," alisema Ferguson.