Huwezi kusikiliza tena

Mwezi mtukufu wa Ramadhan waanza

Jamii ya kimataifa ya kiislamu imelaumiwa kwa kutokuwa mstari wa mbele kukabiliana na majanga ya njaa yanayokumba waumini wengi wa dini hiyo duniani licha ya utajri mkubwa walionao.

Safari hii Ramadhani imeanza huku wengi wa waumini wa dini hiyo katika pembe ya Afrika wanakabiliwa na njaa , ndio sasa jamii hiyo imebidi ijitazame upya.

Michango inakusanywa misikitini ikijumuisha jamii ya Wasomali waishio Kenya.

Jamhuri Mwavyombo amezungumza na katibu mtendaji wa baraza la Maimamu nchini Kenya, Sheikh Khalifa ambae kwanza anafafanua vipi muislamu atatimiza ibada hiyo huku akikabiliwa na njaa