Wapiganaji wa Libya wanasonga

Wapiganaji nchini Libya wamefanya shambulio jipya magharibi mwa nchi.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Baada ya mapambano makali na jeshi la Kanali Gaddafi, sasa inaelekea wapiganaji wameuteka mji wa Bir Ghanem, kama kilomita 80 magharibi ya Tripoli.

Wapiganaji hawakuwahi kufika karibu hivo na mji mkuu, lakini haijulikani kama wataweza kuudhibiti mji. Wapiganaji wanasema sasa wanapanga kujaribu kujongelea mji wa Zawiya ulio kando ya bahari, ambao waliuteka mwanzo wa vita lakini baadaye walitimuliwa na jeshi la serikali.