Fujo zimetokea Tottenham, London

Polisi wa Uingereza wameshambulia watu waliofanya fujo kaskazini mwa London, baada ya kijana mmoja kupigwa risasi na kuuwawa kati ya juma.

Haki miliki ya picha PA

Makundi ya watu yalikusanyika nje ya kituo cha polisi cha Tottenham, na kuchoma moto magari mawili ya polisi pamoja na basi, na kuwarushia polisi mawe, chupa na vyenginevo.

Maduka yalivunjwa na ngawira kuibiwa katika fujo hizo zilizoendelea kwa saa kadha; askari mmoja na waandamanaji kadha walipelekwa hospitali.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri Mkuu, ilisema ghasia hizo hazikubaliki kabisa.

Polisi wanachunguza ghasia hizo, na barabara kati ya mtaa wa Tottenham bado zimefungwa.