Mshukiwa wa mauaji apelekwa A Kusini

Haki miliki ya picha none
Image caption Siku ya harusi ya Dewani

Jaji ametoa uamuzi kuwa mtu mmoja anayetuhumiwa kuamuru kuuliwa kwa mke wake wakati wa fungate nchini Afrika Kusini anaweza kupelekwa ili kesi yake isiskilizwe nchini humo.

Waendesha mashtaka wa Afrika Kusini wamesema wana ushahidi kuwa Srien Dewani alimlipa dereva wa teksi ili aandae mauaji ya mkewe Anni.

Jaji Howard Riddle alisema anaweza kusafirishwa baada ya kusikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Belmarsh mjini London.

Bw Dewani, mwenye umri wa miaka 31, kutoka Bristol, amekana kuhusika kwa namna yeyote na mauaji hayo.

Uamuzi huo lazima uidhinishwe na waziri wa mambo ya ndani Theresa May.

Kundi la wanasheria la Bw Dewani limesema huenda wakakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.