Newcastle, Arsenal nguvu sawa 0-0

Newcastle Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nguvu sawa

Newcastle imetoka sare ya 0-0 na Arsenal katika mchezo uliokuwa na kasoro za hapa na pale.

Katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal kutoka Ivory Coast Gervinho alioneshwa kadi nyekundu baada ya kushikana mashati ya Joey Burton wa Newcastle.

Awali Burton alikanyagwa kwa makusudi na Alex Song, ingawa mwamuzi hakuona tukio hilo.

Arsenal licha ya kujaribu kucheza mtindo wao wa 'kuteleza' walishindwa kuivunja ngome ya Newcastle. Wakicheza bila ya Cesc Fabregas na Samir Nasri, Arsenal walionekana kupata tabu kutengeneza nafasi.