16 wakufa katika shambulio Afghanistan

Ramani ya Afghanistan
Image caption Ramani ya Afghanistan

Watu kama 16 wamekufa katika shambulio lilofanywa na wapiganaji dhidi ya jengo la serikali kati ya Afghanistan.

Watu waliokuwa na silaha pamoja na washambuliaji wa kujitolea mhanga walivamia ofisi za gavana wa jimbo la Parwan Abdul Basir Salangi.

Mapigano yaliendelea kwa saa kadha.

Polisi, maafisa wa usalama na washauri wa kigeni wakihudhuria mkutano hapo wakati shambulio lilipoanza.

Wadadisi wanasema machafuko imezidi hivi karibuni katika eneo hilo.