Shell imedhibiti mafuta yanayovuja

Nembo ya Shell
Image caption Nembo ya Shell

Kampuni ya mafuta ya Shell inasema kuwa imeweza kupunguza mafuta yanayovuja kutoka bomba katika bahari ya kaskazini mwa Uingereza, mwambao wa Scotland.

Tobo hilo lilogundulikana Jumatano, bado halikuweza kuzibwa kabisa.

Shell haikusema kiwango cha mafuta yanayovuja, na serikali ya Uskochi inakisia tani mia moja za mafuta zimeshamwagika baharini.

Makundi ya kutetea mazingira yanalalamika kuwa Shell haikuonesha uwazi katika tukio hilo.