Papa anafanya ibada na vijana

Papa Benedict ameongoza ibada ya mwisho katika sherehe za Siku ya Vijana Duniani, kwenye kituo cha wanahewa nje ya mji mkuu wa Uspania, Madrid.

Haki miliki ya picha AFP

Sherehe hizo za vijana zimekusanya malaki ya vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Hapo jana, hotuba ya Papa kwa vijana ilikatwa kwa sababu ya radi kubwa.

Kofia yake ilichukuliwa na upepo, na mvua ilirovya karatasi ya hotuba yake -- lakini baada ya dhoruba, Papa aliuambia umma kuwa mvua hiyo ilikuwa baraka ya kupooza joto jingi.