Enzi ya Kanali Muammar Gaddafi ukingoni

Muammar Gaddafi Haki miliki ya picha BBC World Service

Baada ya kuiongoza Libya kwa zaidi ya miongo minne, huu huenda ukawa ndio mwisho wa enzi ya Kanali Muammar Gaddafi.

Muammar Gaddafi alizaliwa na wazazi wafugaji kutoka jamii ya Bedouin mwaka wa 1942. Hakupata elimu ya kisasa ila madrassa pamoja na shule ya kijeshi.

Mwaka wa 1969 kanali Muammar Gaddafi aliongoza mapinduzi wakati huo akiwa afisa katika jeshi. Baada ya mapinduzi Gaddafi aliahidi kuleta mageuzi ya kiuchumi, na kuwaondoa wageni aliosema wamethibiti taifa hilo.

Kanali Gaddafi akiwa kiongozi mpya alitaka kandarasi zote kubatilishwa na kutolea chini ya masharti mapya.

Sheria mpya ilifanya Libya kuwa taifa la kwanza masikini kuthibiti biashara ya mafuta, hatua iliyofanya nchi zingine za kiarabu kushinikiza umiliki wa mafuta yao. Miaka ya 70 kukawa na msisimuko wa kiuchumi katika mataifa ya kiarabu yaliyozalisha mafuta.

Kanali Gaddafi alijitangaza kama kiongozi wa waarabu, mfalme wa Afrika, Imam wa Waisilamu na mtetezi wa uhuru wa wanyonge.

Utawala wake umekuwa wa mfumo wa Jumhuri wa Utawala wa wengi. Hapa raia wa Libya wamekuwa wakipitisha sera za serikali bila mpangilio wowote na hakuna aliyekosoa mfumo huo lau sivyo asukumwe jela.

Mummar Gaddaffi na familia yake wamekuwa na ushawishi mkubwa. Mohammed al Gaddafi anaongoza kamati kuu ya Olimpiki na kampuni kadhaa za mawasiliano.

Saif Al Islam ana shahada ya PHD kutoka Taasisi ya kiuchumi ya Uingereza LSE. Alidhaniwa kuwa mridhi wa babake.

Saadi Gaddafi, Mutassim Gaddafi amekuwa mshauri wa masuala ya usalama ya kikosi cha rais.

Hannibal Gaddafi, amekuwa akisimamia kampuni kubwa ya mafuta. Saif al Arab kifunga mimba wa kiume aliuawa kwenye shambulio la NATO mapema mwaka huu nyumbani mwa gaddafi.

Khamis Gaddaffi, ni mwanajeshi na alisimamia vikosi vilivyopambana na waasi huko Benghazi.

Ayesha Al Gaddafi mwana wa kike wa pekee, ni wakili na alimtetea kiongozi wa zamani wa Iraq Saddan Hussein.