Nasri aenda Man City

Manchester City wamekubaliana na Arsenal kumsajili kiungo Samir Nasri. Nasri sasa anaelekea mjini Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nasri

Nasri alifanya mazoezi na Arsenal siku ya Jumanne asubuhi kujiandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Udinese, utakaochezwa Jumatano. Hata hivyo jina lake liliondolewa kwenye orodha ya wachezaji.

Kiungo huyo kutoka Ufaransa anakwenda Manchester pia kukamilisha mkataba wake ambao unadhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25.

Meneja wa City, Roberto Mancini alisema siku ya Jumapili kuwa anataka kumsajili Nasri ndani ya kipindi cha saa 48.