Watu milioni 12 waishi bila utaifa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watoto wasio na utaifa

Takriban watu milioni 12 duniani kote hawana uraia wa nchi yeyote, na matokeo yake kunyimwa haki zao za msingi za kibinadamu, umoja wa mataifa umeonya.

Umoja huo unatoa wito wa nchi nyingine kutia saini makubaliano mawili ya kutokuwa na utaifa.

Umesema hali hiyo inazidi kuwa mbaya kwani watoto wasio na utaifa wanazaliwa na wazazi wasio na utaifa.

Tatizo hilo limeenea zaidi kusini mashariki mwa Asia, Asia ya Kati, Mashariki mwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika.

Antonio Guterres wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi alisema, "Hawa watu wamekata tamaa na wanahitaji msaada kwasababu wanaishi kama vile wamesahaulika kabisa kisheria."

"Mbali na huzuni inayosababishwa kwao wenyewe, athari ya kubagua makundi ya watu vizazi hadi vizazi inasabisha usumbufu mkubwa katika jamii wanazoishi na mara nyingine ndio chanzo cha migogoro."