Mshukiwa wa Kenya akataliwa ombi lake

Image caption Mahakama kuu Uingereza

Mahakama kuu imekataa kuingilia kati kesi ya raia mmoja wa Kenya aliyesema anakabiliwa na kesi ya ugaidi kwasababu hajawasaidia askari wa usalama wa Marekani na Uingereza.

Omar Awadh Omar alisema alichukuliwa kutoka Kenya na kupelekwa Uganda kuhojiwa na maafisa wa nchi za magharibi.

Bw Omar tangu wakati huo amekuwa akishutumiwa kuwa sehemu ya njama nzito iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 70 mjini Kampala Julai mwaka jana.

Lakini mahakama ya London imesema kesi ya Bw Omar si jambo ambalo mahakama za Uingereza zinaweza kuingilia.

Mawakili wa Bw Omar walitaka mahakama kuu kuilzaimisha serikali ya Uingereza kutoa taarifa za madai ya kuwepo mahojiano mwaka jana.

Wamesema mahojiano hayo yanathibitisha kuwa Omar hakukuhusika katika mashambulio ya Julai 2010.