QPR yamuwania Joey Barton wa Newcastle

Kiungo wa Newcastle Joey Barton yupo katika mazungumzo na klabu ya Queens Park Rangers kuhusu uwezekano wa kuhamia klabu hiyo.

Image caption Joey Barton

Barton mwenye umri wa miaka 28, alijiunga na Newcastle mwaka 2007 akitokea klabu ya Manchester City in 2007, mkataba wake unamalizika mwaka huu.

Aliwahi kushutumu sera ya uhamisho za Newcastle na nusura msimu huu asingeichezea klabu hiyo.

Hata hivyo ameweza kucheza mechi zote mbili za ufunguzi wa msimu huu wa Ligi, na katika mechi hizo zote alioneshwa kadi ya manjano.

Mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa msimu huu wa Ligi, alihusika katika purukushani dhidi ya mshambuliaji wa Arsenal Gervinho, na baadae akakiri alijiangusha makusudi katika vurugu hizo, hali iliyosababisha Gervinho atolewe nje kwa kuoneshwa kadi ya manjano katika pambano ambalo timu hizo hazikufungana.

Barton, ambaye aliwahi kuichezea Manchester City na mara moja katika timu ya taifa ya England, wakati huo alioneshwa kadi ya manjano kwa vurugu wakati Newcastle ilipowalaza mahasimu wao wakubwa Sunderland bao 1-0.

Newcastle mara kwa mara imekuwa ikisema Barton yupo tayari kwa uhamisho na hahitaji ruhusa ya kuzungumza na vilabu vinavyomtaka, lakini BBC inafahamu kuwa QPR iliwasiliana na Newcastle kuhusiana na suala la kumchukua Barton.

QPR na Newcastle zitapambana katika mechi ya Ligi Kuu ya England tarehe 12 mwezi wa Septemba.