Naibu katibu wa UN azuru Nigeria

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro, anazuru Nigeria baada ya bomu kuripua makao makuu ya Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa katika mji mkuu, Abuja.

Haki miliki ya picha sahara reporters

Watu kama 19 walikufa katika mripuko huo.

Kikundi cha Waislamu wenye siasa kali, cha Boko Haram, kinasema kilifanya shambulio hilo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, alielezea mripuko huo kuwa shambulio dhidi ya watu wanaotumia maisha yao kusaidia wengine.