Armand Traore wa Arsenal ajisajili QPR

Mlinzi wa kusoto wa Arsenal Armand Traore amejiunga na vijana wapya katika Ligi Kuu ya soka ya England QPR kwa kitita ambacho hakijasemwa.

Image caption Armand Traore

Armand Traore mwenye umri wa miaka 21, anaondoka Arsenal baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka mitano akiwa ameshiriki mechi 23, amesaini mkataba wa miaka mitatu na QPR.

Traore anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na QPR chini ya mmiliki wake mpya Tony Fernandes, akifuatiwa na Joey Barton pamoja na Luke Young.

"Nilipozungumza na meneja Neil Warnock alionekana kuwa na matumaini makubwa nami katika klabu hiyo," alisema Traore.

Traore aliichezea Juventus kwa mkopo msimu uliopita, lakini akawa anatafuta nafasi ya kuwa mchezaji atakayepangwa kila mechi.

Beki huyo atavaa fulana yenye nambari 13 katika klabu hiyo ya magharibi mwa London na Warnock amesema: "Armand amekuwa mchezaji nambari moja niliyekuwa namhitaji kwa muda mrefu.