Viongozi wakutana Paris kuhusu Libya

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mataifa makubwa yakutana Paris kuhusu Libya

Kikao malum kuhusu Libya, ambacho mwenyeji wake ni Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, kinafanyika punde mjini Paris.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton atahudhuria huku China na Urusi, wakilitambua Baraza la Mpito la Libya (NTC) kama serikali halali ya Libya.

Baraza hilo la NTC litaomba msaada wa ulinzi, kuijenga upya Libya na kuandaa kwa ajili ya demokrasia.

Lakini bado halijamkamata Kanali Gaddafi ambaye mtoto wake Saif al-Islam ameapata tena kupigana mpaka kufa.

Mwandishi wa BBC Jon Leyne, akiwa Benghazi, anasema ingawa mkutano wa Paris utakuwa mfupi na uwakilishi, utazipa serikali ambazo zinaliunga mkono NTC nafasi nyingine ya kuonyesha kuwa lina uwezo katika uwanja wa kimataifa.

Anasema mkutano utazingatia mipango ya mpito kuelekea demokrasia, kwa ajilio ya kuijenga Libya upya na mambo kama kuliwezesha kimafunzo jeshi la polisi.

Baraza la NTC, mwandishi wa BBC anasema litashinikiza kuachiliwa zaidi kwa mali ya Libya iliyotiwa tanji lakini litasisitiza kuwa halitaki NATO ipunguze msaada wake wakati ikimalizia kuwaondoa masalia ya vikosi vya Kanali Gaddafi.

Libya, na utajiri wake mkubwa wa mapato yatokanayo na mafuta huku ikiwa na idadi ndogo, si nchi ya kikapuni. Itahitaji mdsaada mkubwa wa kuijenga upya. Hata hivyo kuna wengi walio tayari kuisadia.

Uingereza na Ufaransa, ambazo zilishinikiza kuwa na harakati za kijeshi za anga ambazo ziliongozwa na Muungano wa NATO, wana nia ya kuongoza jukumu la kuijenga upya Libya. Katika mkodno huo, yupo mshirika wa muda mrefu wa Libya barani Ulaya-Italia.