Uturuki yamtimua balozi wa Israili

Ripoti hii haitobadili lolote katika kusuluhisha mahusiano baina ya Uturuki na Israel. Uturuki iliitaka Israili iombe msamaha kufuatia mauwaji ya wakereketwa tisa waliopanda meli kwenda Gaza kuonyesha moyo wa kuunga mkono juhudi za Palestina mwaka jana.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilicheleweshwa mara tatu ili kuwapa mda waIsraili waweze kuomba radhi lakini wakashindwa kufanya hivyo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Bendera ya Israili yachomwa

Kufuatia hali hio, Uturuki sasa inasema kuwa imemtimua Balozi wa Israili kutoka nchini humo na pia kusimamisha uhusiano wa kijeshi. Israili bado haijatoa kauli yake rasmi juu ya Ripoti ya Umoja wa Mataifa ingawa serikali ya Uturuki bila shaka itaridhika nayo.

Ripoti hiyo inasema kuwa Israili ina haki ya kuzuwia shughuli za Gaza za baharini na kwamba jeshi lake la wanamaji lilichukua hatua za kujihami dhidi ya ghasia kutoka Uturuki kupitia meli ndogo.

Hata hivyo, kutokana na ufumbuzi kuwa jeshi la Israili lilitumia nguvu ya kupindukia litawapa Waturuki uzito wa kuweza kufungua mashtaka dhidi ya Makamando wa Israili waliohusika na mauwaji.

Wakati eneo zima la mashariki ya kati likiwa katika hali ya taharuki, nchi hizi mbili zitahitaji kuondoa farakano hii. Hilo ni jambo ambalo huenda likachelewa kufikiwa kwa haraka.