Wapiganaji Libya wajongelea Bani Walid

Wapiganaji wa Libya wanajongelea mji ulioko jangwani wa Bani Walid -- moja kati ya ngome ya mwisho la wanajeshi wa Kanali Gaddafi -- baada ya kutoa ilani kwa mji huo kusallim amri ama sivyo, utashambuliwa.

Haki miliki ya picha AFP

Mamia ya wapiganaji kwenye magari wakiwa na silaha nzito, wanasogelea mji huo kutoka pande tatu.

Lakini mwandishi wa BBC alioko nje ya Bani Walid anasema haijulikani kama wapiganaji wamepewa amri ya kufanya shambulio.

Inafikiriwa kuwa watu wa familia ya Gaddafi pengine wameshakimbia kwa kupitia Bani Walid wakati walipoondoka Tripoli.

Taarifa zinaonesha pengine baadhi yao wangali wamejificha katika mji huo.