Msafara wa Libya wavuka mpaka kuingia Niger

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vikosi vinavyompinga Gaddafi

Msafara wa magari wenye ulinzi na silaha kutoka Libya umevuka mpaka kuingia nchini Niger, ripoti zinasema.

Msafara huo unaaminika ni wa wapiganaji wa Tuareg waliopewa mafunzo na Kanali Muammar Gaddafi aliyekimbia nchi kupigania utawala wake ukielekea katika mji wa Agadez.

Haijafahamika wazi iwapo kuna mwanafamilia yeyote wa Kanali Gaddafi katika msafara huo. Msemaji wake alisema Gaddafi mwenyewe bado yuko Libya.

Kanali Gaddafi ameapa atapigana mpaka kufa, ingawa amepoteza sehemu kubwa ya udhibiti wake nchini Libya.

Nato, ambayo imekuwa ikiendesha harakati za kijeshi za anga kuunga mkono Maamuzi ya Umoja wa Mataifa kuwalinda ria wa Libya, imekataa kusema chochote katika ripoti yake.

'katika ari yahali ya juu'

Msafara huo wenye silaha umevuka mpaka na kuingia Niger na kufika mji wa Agadez Jumatatu, taarifa za kijeshi kutoka Ufaransa na Niger zimelifikia Shirika la Habari la Reuters.

Wamesema msafara huo una magari kati ya 200 na 250 na unasindikizwa na jeshi la Niger.

Wasemaji kutoka Agadez wameiambia BBC kuwa kati ya magari hayo 200, 60 ni ya Libya na yaliyosalia ni kutoka Niger.

Baadaye afisa mmoja kutoka Baraz la Mpito la Taifa Libya (NTC) aliliambia Shirka la Habari la Reuters kuwa msafara huo umebeba dhahabu na fedha na umevuka kuingia Niger kutoka katika mji unaoshikiliwa na Gaddafi wa Jufra.

"Usiku wa Jumatatu, magar 10 yaliyokuwa yamebeba dhahabu, fedha za Euro na dola na kuvuka mpaka kutoka Jufra na kuingia Niger wakisaidiwa na wapiganaji wa Tuaregs kutoka kabila moja Niger," Fathi Baja alisema.

Madai haya hayajathibitishwa na vyombo huru.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Msafara wa waasi

Mwandishi wa BBC Kevin Connolly, aliyeko mjini Tripoli, anasema kuna tetesi kuwa msafara huo unaweza kuwa umebeba washirika wa karibu wa Kanali Gaddafi huku njia ya jangwani inaonekana kuwa ni pekee kuweza kukimbia vikosi vya waasi wanaounda utwawala mpito nchini Libya.

Nchi ya Burkina Faso iliyoko Afrika Magharibi, haina bandari, inachangia mpaka na Niger, imekubali kumpa hifadhi Kanali Gaddafi.

Waasi wengi wa zamani wa Tuareg kutoka Mali na Niger walipewa mafunzo nchini Libya kati ya miaka ya 1970 na 80.

Kanali Gaddafi alisaidia kufikiwa makubaliano ya amani mwaka 2000 kati ya serikali ya Niger na kundi la waasi wa Tuareg linaloongozwa na Rissa ag Boula, ambaye alikimbilia Libya.

Watu wengi walioshuhudia wanasema wamemuona Rissa ag Boula katika msafara huo, lakini amekanusha taarifa hizo akiiambia AFP: "Mimi niko Niamey [Mji mkuu wa Niger]."

Msemaji wa NTC mjini London, Guma el-Gamaty, ameiambia BBC kuwa Niger italipishwa faini iwapo itathibitika kuwa imemsaidia Kanali Gaddafi kutoroka.

"Niger ni jirani na Libya kutoka Kusini na haina budi kufikiria uhusiano wake na Libya siku za usoni," Bw Gamaty alisema. "Hili – iwapo litathibitishwa - litaathiri sana uhusiano kati ya Libya na Niger."

Mke wa Kanali Gaddafi na watoto wake wawili wa kiume na binti yake tayari wamekimbilia Algeria.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mke wa Gaddafi, Safiya na watoto

Mwandishi wa BBC Jon Leyne, mjini Benghazi, yalipo makao makuu ya waasi, anasema kwa msafara mkubwa kama huo usingeweza kukatisha jangwa bila ya Nato kutokuuona.

Nato imekataa kusema chochote kuhusu masuala yake ya kijasusi, msemaji wake ameiambia BBC

Kanali Roland Lavoie amesema kazi kubwa ya muungano wa Nato ni kuwalinda raia sio kufuatlia ‘viongozi wa zamani wanaokimbia nchi, mamluki,makamanda wa jeshi na watu waliopoteza makazi yao ".

Wakati waasi wanaimarisha ngome yao nchini Libya, Nato imeendelea na harakati zake za kijeshi za anga na uangalizi kama ilivyopewa majukumu na UN ya kuwalinda raia wa Libya.

Mapema Jumatatu, msemaji wa Kanali Gaddafi Moussa Ibrahim alisema kiongozi wa Libya ‘yuko vizuri na mwenye ari kubwa’

‘Yuko mahali ambako hataweza kufikiwa na vikundi cha watu tu walioasi nab ado yuko’ Bw Ibrahim ameiambia televisheni ya ya Arrai.