Moto wasambaa kwa kasi Texas

Moto Texas Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moto Texas

Maafisa wanasema kuwa moto umesambaa kwa kasi sana tangu Jumatatu na sasa umeingia katika eneo lenye ekari 25,000.

Gavana wa Texas Rick Perry amekatiza shughuli zake za kampeini ya kugombea kiti cha Rais na kusema kuwa saa 48 na 72 zijazo ni muhimu sana.

Mioto kadhaa imesambaa katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Texas ambayo imechochewa zaidi na upepo mkali wa kimbunga Lee.

Kwa mujibu wa gavana mioto ya hivi majuzi katika jimbo la Texas kwa jumla imeteketeza ekari milioni 3.5.

Gavana Perry amewataka watu wazingatie maagizo ya kuhama na wala wasisalie majumbani kwao ikiwa hawana nguvu za umeme.

Moto katika eneo la mashariki ya Texas ulisababisha kifo cha mama mmoja mwenye umri wa miaka 20 na binti yake siku ya Jumapili kabla ya kuzimwa.