Uchunguzi kwa shabiki aliyeuawa Wembley

Shabiki wa soka wa Wales aliyekufa kabla ya pambano dhidi ya England katika uwanja wa Wembley, ametajwa na mashabiki wenzake kuwa ni Mike Dye, na watu sita wanashikiliwa na plisi kutokana na kifo chake.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Polisi uwanja wa Wembley wakichunguza mauaji

Dye mwenye umri wa miaka 44 alipelekwa hospitali akiwa na majeraha kichwani baada ya kupatwa na maradhi ya moyo nje ya uwanja.

Salamu za rambirambi kwa shabiki huyo wa soka wa klabu ya Cardiff City, aliyefariki dunia usiku wa saa tatu zilitolewa kupitia mtandao wa soka.

Watu hao sita waliokamatwa inaaminika ni mashabiki wa Wales na polisi hawaamini kama kuna shabiki yeyote wa England alihusika na kifo hicho.

Katika taarifa kupitia mtandao wake klabu ya Cardiff City imesema: "Usiku wa Jumanne taarifa zilitufikia kuhusiana na msiba huu ambapo shabiki wa Wales na Cardiff City amekufa katika mechi baina ya England na Wales.

Msemaji wa polisi amesema: "Maafisa wa polisi na wa Huduma za gari la Wagonjwa walimhudumia shabiki huyo. Mtu huyo anayeaminika kuwa na umri miaka 40 alipelekwa hospitalini kaskazini mwa London akiwa na majeraha kichwani. Alitangazwa amekufa saa mbili na dakika hamsini.

England katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu katika Ubingwa wa Ulaya, ilishinda kwa bao 1-0.