Maharamia wawaachia huru mateka

Familia moja ya watu watano na mabaharia wawili kutoka Denmark waliokamatwa na mabaharia wa Somalia mwezi Februari wameachiliwa huru, serikali ya Denmark imesema.

Jan Quist Johansen, mkewe, watoto wake watatu, na watu wazima wengine wawili wamechukuliwa mateka tarehe 24 Februari.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maharamia wa Somalia

Wizara ya mambo ya nje imesema walikuwa katika hali nzuri na kutarajiwa kurejea Denmark hivi karibuni.

Mwezi Machi, askari kutoka eneo lililojitenga la Puntland waliuawa wakati wa jaribio la kuwaokoa watu hao.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo ilisema, "wizara ya mambo ya nje inathibitisha kuwa mabaharia katika meli ya ING- wazazi hao wawili, watoto wao watatu na mabaharia wawili- walishikwa mateka tangu Februari 24, 2011, wameachiliwa huru."

Kikombozi cha dola za kimarekani milioni tatu zilitolewa ili waachiwe huru, ameripoti mwandishi wa BBC wa masuala ya Afrika Mashariki Will Ross.

Wazazi hao wawili, watoto wao-wenye umri kati ya miaka 12 na 16- na mabaharia walikamatwa kwenye bahari ya Hindi walipokuwa wakizunguka maeneo mbalimbali duniani.

Hata hivyo walikuwa wanafahamu hatari ya kuwepo maharamia.

Mashua yao ya anasa yalitekwa siku mbili tu baada ya meli nyingine iliyokuwa na Wamarekani wanne kutekwa na kupigwa risasi na kufa katika jitihada za kuwaokoa zilizofanywa na jeshi la Marekani.

Maharamia wanaendelea kushikilia takriban meli 30 mpaka sasa.