Askofu ataka kukutana na Rais Mugabe

Haki miliki ya picha PA
Image caption Dr Rowan Williams

Askofu mkuu wa Canterbury ameomba wakutane na Rais Robert Mugabe huku kukiwa na ripoti za kuwepo ghasia baina ya makundi yanayopingana ya madhehebu ya Anglikana nchini Zimbabwe.

Dr Rowan Williams anatembelea Malawi, Zimbabwe na Zambia mwezi Oktoba.

Msemaji wake alisema "ziara ya askofu huyo" ni "kuonyesha umoja" na Waanglikana waliopo Afrika ya Kati.

Ofisi ya wizara ya mambo ya nje amesema kama mkuu wa kanisa hilo, Dr Williams' "nia ya kuwaunga mkono inaeleweka".

Dr Williams atakuwa mwakilishi wa kwanza maarufu kutoka Uingereza kutembelea Harare, mji mkuu wa Zimbabwe, katika kipindi cha muongo mmoja.

Mwaka 2007, Askofu mkuu wa York, Dr John Sentamu, alikata kitepe cha shati kinachovaliwa na maaskofu kupinga utawala wa Rais Mugabe, akisema hatokivaa tena mpaka rais huyo aondoke madarakani.