Polisi yazuia mkutano wa wapinzani

Polisi ya kuzuia fujo nchini Uganda imezuia mkutano wa wanaharakati wanaotaka mabadiliko waliokuwa wameuitisha katika uwanja mmoja mjini Kampala wakisema wanaunga mkono wanaharakati wenzao ambao wameleta mabadiliko katika baadhi ya mataifa ya kaskazini mwa Afrika.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Polisi wa Uganda

Maandamano yao yalikusudia kumhimiza kiongozi wa Uganda aondoke madarakani kuepuka kile walichoita fedheha kama kile iliyowapata viongozi wa Libya,Tunisia na Misri.

Raia wengi wa Uganda waliokuwa kando ya sehemu iliotengwa kwa ajili ya mkutano wao karibu na eneo maarufu lijulikanalo kama clock square karibu na kituo cha wazima moto wakisema kuwa Museveni ni lazima atakwenda.

Kelele hizo walizipiga baada ya askari polisi na askari jeshi zaidi ya 300 na ushei kuzingira mahali hapo na kuwazuia kutoingia mahali hapo kufanya mkutano waliouita wa kuonyesha mshikamano na wenzao wa mataifa ya kaksazini mwa afrika ambao waliwashinikiza viongozi wao kuondolewa.

Mkutano huo ambao awali ulikuwa umepangwa kufanyika ijuma iliopita na kuahirishwa baada ya polisi kusem akuwa hautafanyika mahali hapo.Pia na mara hii polisi ilionya kuwa haitakubali kufanyika mkutano mahali hapo ikiwa shauri wandalizi waufanya mahali pengine.

Lakini mwandalizi mkuu mbunge Mathias Mpuuga alisistiza kuwa ataufanya mahali hapo.Na baada ya kusambaza makaratasi yakiwa na picha za ben Ali wa Tunisia,Mubaraka wa Misri,Qadhafi wa Libya na maandishi kuwa ni wakati wa madikteta kwenda ni lazima kuongeza kuwa Museveni ndie aliyebaki alifika mahali hapo na kuanza kuzozana na polisi waliokuwa wanamzuia.

Haikujulikana ikiwa watakutana wakati mwingine na mahali pengine.