11 Septemba, 2011 - Imetolewa 13:22 GMT

Marekani yakumbuka mashambulio ya Septemba 11

Media Player

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Marekani imeanza shughuli za kuwakumbuka waliokufa katika mashambulio ya Septemba 11, miaka 10 iliyopita, katika miji ya Washington na Pennsylvania.

Kuna ulinzi mkali, kufuatia onyo kwamba huenda kundi la magaidi la al-Qaeda likafanya mashambulizi.

Jamaa za waliokufa katika mashambulio ambako ndege nne zilizokuwa zimetekwa na magaidi zilishambulia majumba, na kusababisha vifo vya karibu watu 3,000.

Relatives of those who died are gathering at the sites where four hijacked planes struck, killing nearly 3,000 people.

Kutokuwa na ukumbusho utakaozinduliwa mahali ambapo majengo ya World Trade Centre yalikuwepo.

Vifaa vya kukagua vitu vya chuma vinatumika katika juhudi za polisi za kuwakagua watu wanaofika mahali palikuwepo majengo ya World Trade Centre, huku maafisa wa polisi New York na Washington wakisimamisha magari yanayopita njia za chini kwa chini na daraja katika miji hiyo.

Shirika la Marekani la ujasusi, CIA, wiki iliyopita lilipata habari kwamba huenda kundi la al-Qaeda likawatuma watu kuwashambulia raia wa Marekani, au kuulipua mji mmoja kati ya miji mingi ya Marekani.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.