Kevin Davies amuomba msamaha Cleverley

Nahodha wa Bolton, Kevin Davies amemuomba msamaha Tom Cleverley baada ya kumfanyia rafu mbaya na kumuacha kiungo huyo wa Manchester United akiwa ameumia kano ya mguu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kevin Davies

Mke wa Davies, Emma, aliandika kupitia mtandao wa twitter: "Kwa wale wote waliochukizwa na taarifa hiyo... Kevin amezungumza na Tom Cleverley kwa simu. Kamwe hana nia ya kumuumiza mtu yeyote."

Rafu hiyo mbaya ilifanyika dakika ya tano tu ya mchezo wakati Manchester United walipoilaza Bolton mabao 5-0 na Cleverley hataweza kucheza soka kwa muda wa mwezi mmoja.

Cleverley atakosa kuichezea England katika mechi ya kufuzu Ubingwa wa Ulaya 2012 maarufu Euro, dhidi ya Montenegro mwezi wa Oktoba mbali ya mechi nyingine zitakazoihusu klabu yake ya Manchester United.