Wimbo maarufu wa Malema ‘ni wa chuki’

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Julius Malema

Mahakama kuu Afrika Kusini imeamuru kuwa wimbo wa kupinga ubaguzi ‘ua kaburu’ ni wa chuki na imepiga marufuku Chama cha ANC kuutumia tena.

Kundi la Waafrikana la Afriforum lililalamika kuhusu kiongozi wa Jumuiya ya vijana wa ANC Julius Malema kuuimba wimbo huo ambao unawahusu wakulima wa kizungu.

Bw Malema na viongozi wengine wa ANC walisema kuwa wimbo huo ulikuwa ni kuchagiza vita dhidi ya utawala wa wachache.

Walisema maneno hayo hayakutakiwa kuchukuliwa kirahisi.

Mahakama kuu iliyoa uamuzi huo kuimeamuru Bw Malema kulipa gharama za kuendesha kesi hiyo.

"Maneno hayo ni matusi na ubaguzi, hayana utu," alisema Jaji Collin Lamont, akiongeza kuwa baada ya Afrika Kusini ambayo kwa sasa haina ubaguzi wa rangi, raia wote wanatakiwa kuchukuliwa kuwa wako sawa.

Aliitaka ANC kutafuta namna nyingine ambayo haileti mgawanyiko.

Mwandhishi wa BBC mjini Johannesburg Karen Allen anasema uamuzi huo ni pigo kwa Bw Malema, ambaye aliufanya wimbo huo kama kitambusho chake.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 30 sasa amekuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Jacob Zuma. Kamati ya maadili ya ANC bado inasikiliza shauri la kinidhamu la Bw Malema ambalo huenda limfanya afukuzwe kwenye chama.