Djokovic aonesha ubabe dhidi ya Nadal

Novak Djokovic amethibitisha ubora wake wa kuwa mchezaji bora wa tenis duniani, baada ya kumshinda bingwa mtetezi Rafael Nadal na kunyakua kwa mara ya kwanza taji la mashindano ya US Open.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Novak Djokovic

Mchezaji huyo Mserbia anayeshikilia ubora nambari moja duniani, alionesha mchezo wa kuvutia na kushinda 6-2 6-4 6-7 (3-7) 6-1 katika pambano lililochukua muda wa saa nne na dakika 10 katika uwanja wa Arthur Ashe.

Nadal, ambaye alitazamiwa kushinda taji kubwa kwa mara ya 11, sasa amepoteza mechi zote sita alizokumbana na Djokovic mwaka 2011.

Djokovic anashikilia mataji ya Australian Open, Wimbledon na US Open.

Mara ya mwisho kwa Djokovic kushindwa na Nadal katika hatua ya fainali ilikuwa miezi 12 iliyopita, lakini sasa kibao kimemgeukia Nadal.