Uchumi kukwama Ulaya

Tume ya Ulaya imebashiri kuwa ukuaji wa uchumi katika eneo la Ulaya utakwama katika miezi iliyosalia ya mwaka 2011.

Image caption Kamishna wa Muungano wa Ulaya kuhusu masuala ya uchumi, Olli Rehn

Tume hiyo imepunguza makadirio yake ya awali ya ukuaji kwa mwezi Julai hadi September kwa asilimia 0.2, ihali kwa miezi mitatu ijayo imepunguza makadirio ya ukuwaji kutoka asilimia 0.4 hadi 0.1

Tume hiyo imesema haya yanasababishwa na msukosuko uliokumba masoko katika msimu wa majira ya joto ikiwa ni pamoja na kupungua kwa uwagizaji bidhaa kutoka nje ya Ulaya.

Lakini tume inasema bado ina imani hakutakuwepo na mdororo wa uchumi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa wanachama wa Muungano huo, ambao wamelazimika kubana, uchumi wao pia utakua.

Moja ya nchi ambazo zinabana matumizi ni Ugiriki ambayo imekariri jana kuwa imejitolea kuzingatia mipango yote ya kubana matumizi ili nayo kwa upande wake ipate kusaidiwa.

Kumekuwa na wito wa kuunga mkono Ugiriki, hatua ambayo imenyanyua masoko ya hisa hii leo.

Viongozi wa Ulaya wamesema kuwa Ugiriki ni muhimu sana katika eneo la Ulaya.

Ugiriki inajiandaa kupokea mkopo mwengine kutoka Muungano wa Ulaya na Shirika la Fedha Duniani IMF baadae mwezi huu, lakini hili litafanyika tu iwapo wakaguzi kutoka Muungano wa Ulaya,Benki Kuu ya Ulaya na IMF zitakapokubaliana kuwa nchi hiyo inazingatia mpango wa kupunguza na kubana matumizi kama inavyotakiwa.