Mataifa mengi 'hayatofikia malengo'

Watafiti wamesema nchi tisa tu kati ya 137 zilizoendelea zitafikia malengo yao ya kuimarisha afya ya wanawake na watoto.

Tathmini hiyo ilmetolewa kwenye jarida la Lancet likionyesha maendeleo ya hivi karibuni ya malengo ya milenia (MDG) ya nne na tano.

Wataalamu wanatabiri kuwa hakuna nchi yeyote kusini mwa jangwa la sahara itakayofikia malengo ya kupunguza vifo ifikapo mwaka 2015.

Lakini limesema maendeleo yanaongezeka kwa kasi katika nchi nyingi.

Malengo hayo yalifikiwa na viongozi duniani mwaka 2000.

MDG4 ina dhamira ya kupunguza idadi ya watoto wanaofariki dunia wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa robo tatu kati ya mwaka 1990 na 2015.

MDG5 inaelezea kuwa na nia ya kufuta vifo miongoni mwa wanawake wajawazito kwa kiwango cha robo tatu katika kipindi hicho hicho.

Watafiti hao kutoka Seattle wanakadiria kuwepo vifo vya watoto wachanga milioni 7.2 duniani kote katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita- ikilinganishwa na watu milioni 11.6 mwaka 1990.

China, Rwanda na Botswana wamesifiwa kwa "kasi" katika kupambana na vifo vya watoto kwa muongo mmoja uliopita.