Mfuasi wa Haqqani akamatwa Afghanistan

Kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na NATO nchini Afghanistan, ISAF, kinasema kuwa kimemkamata mmoja kati ya viongozi wa kikundi cha wapiganaji cha Haqqani, ambacho kimelaumiwa kwa mashambulio kadha nchini.

Haki miliki ya picha Reuters

ISAF inasema Haji Mali Khan alikuwa amejihami na silaha kubwa, lakini hakufanya ukaidi alipokamatwa, pamoja na wapiganaji wengine.

ISAF imeeleza tukio hilo kuwa muhimu katika juhudi za kukichafua kikundi hicho cha Haqqani, ambacho inasema kilifanya shambulio la karibuni dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Kabul.

Kikundi hicho ndio tawi kali kabisa la Taliban, ambao wamekanusha kuwa Mali Khan amekamatwa.

Mali Khan, mjomba wa Siraj na Badruddin Haqqani, anasemekana kuwa ndiye aliyeanzisha vituo vya wapiganaji mashariki mwa jimbo la Paktia, na kupanga mashambulio ya kujitolea mhanga katika mji mkuu, Kabul.