NTC yaombwa kuzuia mateso ya wafungwa

Shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch, limetoa wito kwa Baraza la Mpito nchini Libya, NTC kuagiza makundi yaliyojihami kukoma kuwakamata watu kiholela na kuwahujumu wafungwa nchini humo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kiongozi wa Baraza la Mpito nchini Libya

Shirika hilo lilizuru magereza 20 na kusema kuwa limepokea ripoti kuwa wafungwa sita waliteswa katika vituo vinavyosimamia na wanajeshi watiifu kwa Baraza la Mpito NTC.

Walinzi katika vituo hivyo wanatuhumiwa kuwadhulumu wafungwa katika magereza hayo ya muda kwa kuwapiga viboko na hata kutumia umeme.

Shirika hilo linasema wafungwa wanaotuhumiwa kuhusika na visa vya ubakaji na mauaji walionekana kudhulumiwa zaidi na kushurutishwa kukiri mashtaka dhidi yao na walizi katika magereza hayo.

Shirika hilo la Human rights watch, limetoa wito kwa Baraza hilo la Mpito, kubuni mfumo wa haki ambao utahakikisha kuwa wafungwa wote wanapewa haki.