Aliyemuuwa Rabbani ni Mpakistan

Taarifa ya ofisi ya rais wa Afghanistan imeeleza kuwa mtu aliyemuuwa rais wa zamani wa Afghanistan, Burhanuddin Rabbani, ni raia wa Pakistan.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Bwana Rabbani - ambaye akijaribu kupatanisha baina ya serikali ya Afghanistan na wapiganaji wa Taliban - aliuliwa wiki mbili zilizopita na mtu aliyejitolea mhanga.

Kikundi cha wahalifu cha Haqqani kililaumiwa kwa mauaji hayo, kikundi ambacho Marekani inasema kinadhibitiwa na idara ya ujasusi ya jeshi la Pakistan.

Na waandishi wa habari wanasema kisa hicho kimezidi kuharibu uhusiano baina ya serikali za Afghanistan na Pakistan.