Murray ashinda mashindano ya Thailand

Mcheza tennis wa Uingereza Andy Murray alimzidi kwa kila hali Mmarekani Donald Young na kupata ushindi wa mashindano ya Thailand Open kwa 6-2 6-0 katika mchezo uliocheza kwa dakika ya 48.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Andy Murray

Murray alianza kwa kushinda michezo minne ya mwanzo kabla Young hatimaye kuzinduka, lakini Murray alifanikiwa kushinda seti ya kwanza.

Young ambaye anashikilia nafasi ya 55 ya ubora wa wacheza tennis duniani, hakufurukuta hata kidogo katika mchezo wa pili huku Murray ambaye alimshinda Mmarekani huyo katika mchezo wa US Open, akijipatia taji la tatu msimu huu.

Murray mwezi wa Machi katika mashindano ya Indian Wells alifungwa na Young

"Hii ilikuwa ni fainali yangu ya kwanza, sikuwa na wasiwasi, lakini aliniwahi katika mchezo ule, alisema Young, ambaye anatazamia kupanda daraja la ubora kwa wacheza tennisi duniani na kuwemo miongoni mwa wachezaji bora 50, orodha itakapotangazwa siku ya Jumatatu.