Haqqani: Hatukushiriki mashambulio Afghanistan

Image caption Siraj Haqqani: Kiongozi wa wapiganaji wa Haqqani

Kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Haqqani nchini Afghanistan amedai kuwasiliana na mashirika ya ujasusi ya Marekani ambayo yamemshinikiza kufanya mazungumzo ya amani na serikali ya nchi hiyo.

Siraj Haqqani ameyafichua haya katika mahojiano ya kipekee na shirika la utangazaji la BBC, hata hivyo hakuelezea jinsi alivyojibu pendekezo hilo.

Kuhusu mashambulio ya hivi majuzi mjini Kabul amesema yalipangwa na baraza la kijeshi lililoteuliwa na kundi la Taliban ambalo pia hutoa amri kwa wapiganaji wake.

Amekanusha kuwepo ushirikiano kati ya kundi la Haqqani na shirika la ujasusi la Pakistan tangu Urussi kuivamia Afghanistan miaka ya themanini licha ya Marekani kudai kuwa wanashirikiana.

BBC inaamini mahojiano haya ni ya hakika.

Matamshi yake yalinaswa kwenye ukanda wa sauti akijibu maswali aliyoandikiwa na kitengo cha Pashto cha idhaa ya dunia ya shirika la utangazaji la Uingereza, BBC