''Kagame aliamuru kudunguliwa ndege"

Image caption Rais Paul Kagame wa Rwanda

Aliyekuwa mshirika wa karibu na sasa mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame wa Rwanda amemshutumu Rais huyo kwa kuhusika katika mauaji ya Rais wa zamani.

Theogene Rudasingwa anadai amemsikia Rais Kagame akijigamba mara nyingi kwamba aliamrisha kudunguliwa kwa ndege iliyokuwa imembeba kiongozi wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana mnamo mwaka 1994.

Tukio hilo lilizusha mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu laki nane wengi wao wakiwa watutsi walio wachache.

Kagame amekanusha mara kwa mara kuhusika katika mashambulio hayo.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa Rudasingwa amekuwa mkosoaji mkubwa wa Kagame katika miaka ya hivi karibuni na amehukumiwa kifungo kirefu gerezani kwa tuhuma za ugaidi licha ya kutokuwepo nchini humo.