Uchina na Urusi zapinga azimio la UN dhidi ya Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption UN yashutumu Syria kwa kutumia nguvu kuzima maandamano

Uchina na Urusi wametumia kura zao za turufu kupinga azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililoshtumu Syria kwa kutumia nguvu kukabiliana na waandamanaji wanaopinga serikali.

Mataifa tisa waliunga mkono azimio hilo lililoandaliwa na nchi za Ulaya katika baraza hilo la nchi 15, nchi nne hazikupiga kura.

Azimio hilo lilihitaji wingi wa kura ili kuidhinishwa, bila upinzani kutoka kwa wanachama wa kudumu katika baraza hilo.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 2,700 wameuawa nchini Syria tangu maandamano hayo kuanza mwezi wa tatu.

Serikali ya Rais Bashar al-Assad inasema iko kwenye mchakato wa kuanzisha mageuzi na wanazungumza na upinzani.Wanalaumu makundi yenye silaha kwa kusababisha hali ya wasiwasi nchini humo.

'jambo lisilokubalika' Azimio hilo - ambalo lililoandaliwa na Ufaransa kwa ushirikiano wa Uingereza, Ujerumani na Ureno - lilikataliwa wakati wa mchakato wa kupiga kura katika Umoja wa Mataifa jijini New York.