Mwanamke ajichoma moto Algeria

Mwanamke mmoja wa Algeria, amekufa baada ya kujichoma moto akiwa pamoja na mtoto wake wa kiume wa miaka mitatu, walipotimuliwa kutoka fleti yao.

Haki miliki ya picha AFP

Vyombo vya habari vya huko vinaarifu kuwa mwanamke huyo mjane mwenye watoto wawili, na hakuwa na kazi, alilazimishwa kutoka katika fleti yake katika mji wa Oran, kwa sababu aliinunua bila ya kuwa na nyaraka zote zinazotakiwa.

Mtoto wake wa kiume aliungua vibaya lakini amenusurika. Tukio hilo linakumbusha kisa cha mchuuzi aliyejichoma moto nchini Tunisia mwaka jana, na kuwa chanzo cha maandamano makubwa katika karibu nchi zote za Kiarabu.