Mashambulio yaendelea Sirte, Libya

Majeshi ya serikali ya Libya wanaendelea na mashambulio dhidi ya kati ya mji wa Sirte, ngome ya Gaddafi.

Haki miliki ya picha Reuters

Makamanda wanasema bado wamedhibiti maeneo waliyoyateka jana, lakini wanasubiri kufanya shambulio jengine kwa vifaru na mizinga kabla ya kusonga mbele zaidi, na kuteka maeneo ya wafuasi wa Kanali Gaddafi.

Madaktari wanasema watu kama 12 wameuwawa na wengine zaidi kujeruhiwa tangu wapiganaji kuanza mashambulio makubwa dhidi ya Sirte, mji alikozaliwa Gaddafi.