Rais wa Yemen asema ataondoka

Rais wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, amesema ataondoka madarakani katika siku zijazo.

Haki miliki ya picha AFP

Katika hotuba iliyoooneshwa kwenye televisheni ya taifa, Rais Saleh alisema yeye hana uchu wa madaraka, lakini hakutoa tarehe ya kung'atuka.

Rais Saleh amewahi kutoka ahadi kama hiyo, wakati wa miezi ya maandamano dhidi ya utawala wake, lakini aliahirisha dakika ya mwisho.

Mwanaharakti wa Yemen aliyepewa tuzo ya amani ya Nobel juma hili, Tawakul Karman, anasema upinzani hauamini maneno ya rais.

Lakini naibu waziri wa habari aliiambia BBC kwamba Rais Saleh sasa hang'ang'anii tena madaraka.