El Bashir na Salva Kiir waafikiana

Serikali ya Sudan mjini Khartoum imeweka tarehe maalumu ya kufikia suluhu juu ya matatizo na jirani yake, Sudan Kusini.

Haki miliki ya picha Reuters

Rais Omar al Bashir alisema amezipa kamati muda wa kushughulikia maswala yote.

Rais Bashir alitoa tangazo hilo katika mkutano wa waandishi wa habari, akiwa pamoja na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, ambaye anazuru Khartoum kwa mara ya kwanza tangu nchi yake kupata uhuru miezi mitatu iliyopita.

Uhusiano baina ya nchi mbili hizo uliharibika kwa sababu ya hitilafu kadha kuhusu mgao baina yao wa pato la mafuta, na mipaka yao.

Viongozi wote wawili wamekariri kuwa wanataka kushirikiana kuleta amani.