Liverpool yataka vilabu kumiliki haki TV

Mashabiki wa Liverpool Haki miliki ya picha PA
Image caption Mashabiki wa Liverpool

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Liverpool amesema vilabu vya Premier League vya England viwe na uwezo wa kufanya mikataba yao wenyewe ya televisheni nje ya nchi.

Ian Ayre ameonesha wasiwasi kwamba vilabu vya soka vya England vitaachwa nyuma na wenzao wa Ulaya iwapo mapato ya nje yataendelea kugawanyawa sawa baina ya vilabu 20 vinavyoshiriki ligi.

Ayre amesema: "Vilabu vingine vya Ulaya kamwe havifuati mfumo huo. Wapata mapato makubwa kuwawezesha kuzunguka huku na huko kununua wachezaji wazuri."

Mikataba ya haki za kuonesha nje mechi za Premier League, yenye thamani ya paundi bilioni 1.4 inamalizika mwaka 2013.

Chini ya utaratibu wa sasa, timu 14 zitahitajika kupiga kura kuidhinisha makubaliano yoyote mapya.

Ayre anaamini kwamba Liverpool - pamoja na Manchester United, Chelsea na Arsenal - zinapaswa kupokea kiwango cha juu cha mapato.

Nchini Hispania, Barcelona na Real Madrid wana uwezo wa kujadiliana juu ya mikataba yao, ikiwa na maana wanaweza kupata mapato zaidi kulinganisha na vilabu vingine vinavyoshiriki ligi ya nchi hiyo - La Liga.

Na Ayre akaonesha matatizo yanayojitokeza kuwa na mikataba ya muda mrefu: "Iwapo tutaendelea kugawana sawa mapato, mnatunyima haki yetu."

Ameiambia BBC mjini Liverpool: "Ni mjadala unaohitaji kujadiliwa kwa usawa kwa manufaa ya vilabu vya Premier League.