Mataifa ya kiarabu na Afrika Kaskazini

Vuguvugu la kutaka mabadiliko Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Vuguvugu la kutaka mabadiliko

Taarifa mpya zasema maandamano ya wengi mwaka huu kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati kutaka mabadiliko katika sera na utawala yameligharimu eneo hilo dola bilioni 50.

Taarifa hiyo iliyotolewa na kundi la Geopolicity, inasema kuwa Misri na Libya ndio zimepata hasara kubwa zaidi.

Taarifa hiyo imeonya bila ya kuwepo msaada wa kimaeneo, matokeo ya vuguvugu hilo huenda yakaleta hasara kubwa. Nchi zinazozalisha mafuta ambazo zimeepuka maandamano hayo zimefaidi zaidi kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Kwa kuzingatia takwimu za shirika la fedha duniani IMF, kundi hilo limesema nchi ambazo zimekabiliwa na ghasia ama mzozo wakati wa vuguvugu la kutaka mabadiliko zinatarajiwa kupata hasara kubwa katika kipindi kifupi.

Libya, Syria, Egypt, Tunisia, Bahrain na Yemen zimepata hasara kubwa kiuchumi. Gharama katika kiasi cha mapato ya kitaifa inafikia dola bilioni 20.56 ilhali jumla ya pesa za umma ni dola bilioni 35.28.