G20 wamaliza mkutano

Mawaziri wa fedha wa mataifa yanayoongoza kiuchumi ya G-20 wamemaliza majadiliano yao kuhusu matatizo ya madeni ya nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya Euro.

Haki miliki ya picha AFP

Waziri wa Fedha wa Ufaransa, Francois Baroin, amesema matokeo ya mkutano wa kilele wa Ulaya baada ya juma, yatakuwa thabiti katika kukuza uchumi wa dunia.

Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne, alisema kulikuwa na shime kwenye mkutano.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Tim Geithner, alisema amatiwa moyo na maneno yaliyosemwa mkutanoni kuhusu mpango mpya.

Mpango huo utazidisha uwezo wa mabenki, kupunguza deni la Ugiriki, na kuzidisha mfuko wa kusaidia nchi za Euro.