Malalamiko juu ya uchaguzi wa Liberia

Vyama vikuu vya upinzani vya Liberia vimelaani uchaguzi wa rais uliofanywa Jumaane, kwamba ulikuwa wa udanganyifu.

Haki miliki ya picha Reuters

Matokeo yaliyotoka hadi sasa yanaonesha rais wa sasa, Bibi Ellen Johnson Sirleaf, anaongoza kidogo lakini bado hakupata kura za kutosha za kuepuka duru ya pili.

Vyama vinane, kikiwemo cha mpinzani mkuu, Winston Tubman, vinasema shughuli za kuhesabu kura zina dosari.

Bwana Tubman aliiambia BBC kuwa kulitokea ulalamishi katika karatasi za kura na masanduku ya kura yalifunguliwa mapema.

Alisema vyama vya upinzani havitatoka katika uchaguzi kabisa, lakini vinataka tume ya uchaguzi ishughulikie malalamiko yao.