Huwezi kusikiliza tena

Tanzia ya Kanali Muammar Gaddafi

Kuondolewa kwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi kufuatia mapinduzi ya kiraia kumehitimisha utawala wa kiongozi huyo wa Kiarabu aliyekaa kwenye madaraka kwa muda mrefu zaidi.

Kanali Gaddafi aliingia madarakani nchini Libya mwaka 1969. Alikuwa siku zote ni kiongozi mwenye misimamo yake na mwenye utata Mashariki ya kati, Afrika na nchi za magharibi.

Kwa miaka mingi serikali nyingi zilikuwa zikimchukulia kama mtu aliyeunga mkono ugaidi.

Hata hivyo katika mabadiliko ya ghafla ya kisera mwaka 2003 alisalimisha silaha za maangamizi makubwa na akajikuta akisifiwa sana na wanasiasa wa magharibi kama mtu wa watu.

Mwaka 2011 alikumbana na maandamano ya watu wanaompinga kutoka ndani ya Libya. BBC inaangazia safari ya maisha yake na taaluma yake.