Mbunge wa Uingereza ajiuzulu

Mike Hancock alikutana na Katia Zatuliveter alipohudhuria mkutano mjini Moscow. Baadaye bibi huyo alifanya kazi kwa mbunge huyo katika bunge na baadaye kuwa mpenzi wake.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Katia Zatuliveter

Serikali ya Uingereza inadai kuwa alikua akifanya kazi kama jasusi was Urusi na kumlenga Bwana Hancock kwa sababu ya madaraka yake kwenye kamati ya Ulinzi ya bunge.

Amekanusha kua amewahi kumruhusu kuona hati na masuala muhimu ya siri lakini amejiuzulu kutoka wadhifa wake kwenye kamati hio.

Wakati huo huo, Bi Zatuliveter anasema kua inasikitisha kurushiwa tuhuma kua ni jasusi, ingawa kesi yake imekua ikisikilizwa juu ya jinsi alivyokua na uhusiano na wanaume wengine wenye madaraka-akiwemo afisa wa NATO pamoja na mwanabalozi wa Uholanzi.