Zambia yaiomba radhi Angola kwa ‘uhaini’

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2011 - Saa 17:47 GMT
Rais Sata na wananchi wa Zambia

Rais Sata na wananchi wa Zambia

Zambia imewaomba radhi Angola kwa ‘uhaini’ iliofanya kuwaunga mkono waasi wa zamani waliopigana na serikali ya Luanda wakati wa vita.

Rais mpya aliyechaguliwa Michael Sata alisema ametuma ujumbe Luanda kuomba radhi kwa Rais.

Katika miaka ya 1990, Angola iliituhumu Zambia kwa kuwaunga mkono waasi wa kundi la Unita – tuhuma ambazo Lusaka imelikanusha.

Hatua ya Bw Sata ni sera ya hivi karibuni ya Zambia tangu ashinde uchaguzi mwezi uliopita.

Bw Sata alisema amempeleka Rais wa kwanza wa Zambia, Kenneth Kaunda, kuomba radhi kwa Rais wa Angola Angola, Jose Eduardo Dos Santos.

'Kumsaidia Savimbi'

"Nimepeleka ujumbe wangu maalum kabisa kwenda kuomba radhi kwa Rais,"

Rais wa Zambia Michael Sata

Bw Sata amesema hayo wakati akipokea nyaraka za balozi mpya wa Angola Balbina Malheiros Dias Da Silva.

Alisema Zambia wakati wa utawala wa Bw Fredderick Chiluba, aliyefuata baada ya Rais Kaunda, ilifanya uhaini kwa kumuunga mkono kiongozi wa waasi Jonas Savimbi.

Vikosi vya Angola vilimuua Bw Savimbi mwaka 2002, na kumaliza ukatili wa vita ambavyo vilidumu tangu uhuru mwaka 1975.

Serikali ya Bw Chiluba ilikanusha kwa nguvu kumsaidia Bw Savimbi.

Bw Sata alishika madaraka mwezi Septemba baada ya kumshinda mtangulizi wake Rupiah Banda, katika uchaguzi.

Aliapa kudhibiti ufisadi na kutikisa mfumo mzima wa kisiasa.

Tayari ameshafuta kuuzwa kwa mojawapo nchini Zambia, Finance Bank, iliyokuwa iuzwe kwa First Rand ya Afrika Kusini.

Bw Sata pia ametaka Malawi iombe radhi baada ya kumkamata na kumrudisha nchini mwaka mwaka 2007.

Kurejeshwa kwake kulifuatia tuhuma kuwa alikuwa anapanga mapinduzi nchini Malawi, madai ambayo ameyakanusha vikali.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.