Jenerali wa Algeria akamatwa Uswiswi

Maafisa wa mashtaka wa Uswiswi wameanza uchunguzi kuhusu waziri wa ulinzi wa zamani wa Algeria, anayeshukiwa kuhusika na uhalifu wakati wa vita.

Haki miliki ya picha Getty

Ripoti zinasema Khaled Nezzar anashutumiwa kufanya ukatili wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Algeria katika miaka ya 1990.

Alikamatwa juma hili alipokwenda kutibiwa nchini Uswiswi.

Jenerali huyo aliyestaafu, mwenye umri wa miaka 74, alihudhuria kikao cha awali cha kesi yake hapo jana.